Saturday, 21 June 2014
Mwanamke wa Kitanga ndani ya Daladala Balaa Tupu
Hawa wanawake wa kitanga wamezid jamani heeeeee.....
Alikuwa kapanda na bwanake kwenye daladala wamekaa siti moja, mwanamke
kamchukua bwanake akamuegesha kwenye kifua chake akawa anamuimbia nyimbo
za kimahaba, halafu sio kwa sauti ya chini chini ilikuwa sauti kubwa tu
mpaka kila mtu akawa anashangaa.
Alipokuwa anashuka akasema "mi ndio mtoto wa kitanga, nimefundwa
nikafundika wenye kununa wapasuke twende tukalale laazizi wangu"
hahahahahaha
AUNT EZEKIEL: Bado Sijaona Mwanaume wa Kunizalisha
Wakati rafiki yake kipenzi, Wema Sepetu akidaiwa kunasa mimba ya
Diamond , Aunt Ezekiel yeye amesema bado hajaona mwanaume
anayeweza kumtia mimba na hatimaye kuitwa baba wa watoto wake.
Akipiga stori na mwanahabari wetu , Aunt Ezekiel amedai kuwa
kuna wakati unaweza kumuona yupo kwenye ndoa au uchumba lakini
haimaanishi kuwa kuwepo katika mazingira hayo ndo anaweza
kuzaa au kushika mimba kwani suala hilo kwake ni kubwa sana
na hajafikiria kama linaweza kutokea kwa sasa…
“Siyo kwamba sina uwezo wa kubeba mimba, hapana, suala kubwa hapa ni kwamba bado sijaona mwanaume wa kunizalisha.
“Ni kweli nilikuwa kwenye ndoa lakini sikutaka kubeba mimba na
ndo maana hadi sasa hivi nipo kama ninavyoonekana,” alisema
Aunt Ezekiel.
Subscribe to:
Comments (Atom)




