Shule Binafasi Zajitokeza na Kumpongeza Waziri wa Elimu Kwa Kufuta Mfumo wa GPA na Kurudisha wa Division
Shirikisho la wamiliki wa shule na vyuo visivyo vya serikali TAMONGSO
watoa pongezi kwa Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia
na Ufundi kwa kuliagiza Baraza la Taifa la Mitihani kufuta mfumo
unaotumika sasa wa Wastani wa Alama (GPA) na kurudi katika mfumo
uliokuwa unatumika hapo awali wa division.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti
Taifa wa TAMONGSO Bwa. Mrinde Mzava amesema kuwa Waziri wa Elimu
Ameitendea haki Sekta ya Elimu kwani mfumo huo ulileta sintofahamu kwa
wananchi wengi.

No comments:
Post a Comment