Kaburi la mmoja kati ya watu waliopoteza
maisha katika ajali mbaya iliyohusisha mabasi
ya Mwanza Coach na J4
katika eneo la Sabasaba, Musoma, Mara limekutwa likiwa limefukuliwa na
watu wasiojulikana leo asubuhi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichofika
katika eneo la makaburi ya Musoma Basi, ndugu wa marehemu aliyetajwa kwa
jina la Juma Sai walienda asubuhi kuangalia kaburi ikiwa ni siku ya
tatu tangu wafanye mazishi, ndipo walipokuta kaburi limefukuliwa na mbao
zilizotumika kuhifadhi mwili kwa imani ya dini ya kiislamu zikiwa
zimewekwa pembeni.
“Mwili wa marehemu bado uko ndani, watu
wengi wako hapa na polisi wameimarisha hali ya usalama. Madaktari
wameshafika hapa na wanafanya uchunguzi kuona kama kuna kiungo chochote
kilichotolewa kwenye mwili wa marehemu. Inasikitisha sana.” Kimeeleza
chanzo chetu cha kuaminika.
Ijumaa iliyopita, kulitokea ajali mbaya
iliyohusisha magari matatu, mabasi ya kampuni ya Mwanza Coasch na J4
pamoja na gari dogo aina ya Landcruiser. Watu zaidi ya 40 walifariki na
wengine 79 kujeruhiwa
No comments:
Post a Comment