Home /
Music,
Slider
/
Alikiba: Sina bifu na Diamond lakini alinikosea na nikaumizwa na nilisha samehe
Alikiba: Sina bifu na Diamond lakini alinikosea na nikaumizwa na nilisha samehe
Music, Slider 8:33 AM
Msanii Alikiba ameamua kufungaka na kuweka waZi kili kinacho hitwa
tofauti au bifu kati yake na Msanii Diamond!Kwanza lazima tukubaliane
kuwa ALikiba ni mmoja wa Wasanii wasio penda maneno na malumbano na
wasanii wenzie ndio maana hukaa kimya. Kwanza Alikiba alisema hana bifu
na diamond na hana sababu ya kuwa na bifu nae japo yanayo ongelewa yana
muumiza sana na aliamua kuondokana na hayo yote busara ya haraka ilikuwa
kukaa kimya.
Aliendelea kusema aliumizwa sana aliposikia kuwa amefuta mistari ya
diamond kwenye wimbo wa Single boy ambao aliimba na lady jaydee na
hakuimba kabisa na diamond na hata producer aliye record wimbo huo
alithibitisha. Aliendelea kusema kuwa aliumizwa sana na uongo huo kuhusu
yeye na hakupenda kuuongelea sana kwa sababu ange onekana anatafuta
kick wakati hakuKuwa na kitu kama hicho.
Pia Alikiba aliamua kusema kuwa aliumizwa sana na kitendo cha Diamond
kufuta mistari yake kwenye wimbo wa Lala salama maana Diamond
hakumwambia kwanini kafanya hivyo na hadi leo hakuwai kumwambia. Alisema
hilo swala amechukulia kama na Kitendo cha mtu kuomba mtihani wako
aangalizie alaf baadae ana kurudishia mtihani wako na kusema sitaki
majibu yako au ana yafuta yote alaf unategemea atajisikiaje? na alisema
yeye alisha samehe lakini Diamond alimkosea na hadi leo hawakuwai
kukutana.
No comments:
Post a Comment